DILLISH AMKANA MWANAUME WA KENYA ALIYEDAI KUWA DILLISH NI MWANAE..
Baada ya mwanaume mkenya Abdi Galgayo
Guyo aliyejitokeza juzi katika ofisi za Standard Media Kenya na kudai
kuwa ndiye baba mzazi wa mshindi wa BBA The Chase Dillish Mathews kutoka
Namibia, Dillish amemkana na kusema baba yake ana asili ya Somalia.
Mashabiki mbalimbali wamemuuliza Dillish kuhusu Guyo kupitia twitter, lakini Dillish ambaye ameonesha kushangazwa na habari hizo, jana alitweet kuwa baba yake ana asili ya Somalia hivyo hajui huyu jamaa ameibukia wapi!..

Bwana Guyo ambaye ni askari mstaafu wa
Kenya alisema alikuwa ni miongoni mwa maaskari wa Kenya wa kikosi cha
kulinda amani cha Umoja wa mataifa ‘United Nations Transition Assistance
Group ‘, kilichopelekwa nchini Namibia kuanzia (April 1989) mpaka
(March 1990) kusimamia mchakato wa amani pamoja na uchaguzi wa kwanza wa
nchi hiyo na huko ndiko alikutana na mama yake Dillish aitwaye Selma na
wakapendana.
Kwa mujibu wa Standard Media,
wiki iliyopita mwandishi wa Namibia Rinelda Mouton alifanya mahojiano
maalum na Dillish Mathews, ambaye alisema anatamani kukutana na baba
yake mzazi.
0 comments: