VURUGU KUBWA ZAZUKA LEO MWANZA, POLISI WAPAMBANA NA WAFUASI WA CHADEMA..!
Maandamano ya chama cha CHADEMA yaliyokua yanafanyika huko mwanza
yamegeuka vurugu baada ya wandamanaji kuanza kupambana na polisi.
CHADEMA walikuwa wakiandamana katika kushinikiza Meya wa Ilemela Henry
Matata aachie ngazi kwani hana sifa zakua meya, baada ya kuvuliwa
uanachama na chama hicho.
Katika picha zilizokirushwa kupitia televisheni ya Barmedas Tv ya
Mwanza, barabara zimeonekana zikiwa zimefungwa kwa mawe na miti, huku
katika maeneo mengine uchafu ukiwa umejazwa barabarani na matairi
kuchomwa.
Katika mtaa wa Mission waandamanaji wamefunga barabara kwa uchafu uliokua katika dampo moja kando ya barabara hiyo.
Maandamano hayo yalikuwa yamalizikie viwanja vya Furahisha ambapo viongozi wa CHADEMA walitarajiwa kuhutubia.
Hivi sasa polisi wametanda mitaani katika kudhibiti vurugu hizo na hali inaonekana kutengamaa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: