Msanii nyota kwenye tasinia ya muziki na filamu bongo Zuwena Mohamed “
Shilole” mwishoni mwa wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya
kutiwa mtu kati na wakina dada waliokuwa wanamdai kiasi kikubwa cha
pesa.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na mmoja wa wakina dada
hao waliokuwa wanamdai zilisema kuwa wanawake hao waliamua kuchukua
hatua za kumtia adabu Shilole baada ya kupata taarifa kuwa siku hiyo
alikuwa ana hama kwa kukimbia na teni lao
“ Ishu ilikuwa hivi
sisi tunamdai huyu dada lakini cha kushangaza amekuwa akitupiga chenga
sana na ona alivyokuwa sio mstaarabu kumbe siku hiyo alikuwa anahama na
deni letu ndio maana tuliamua kwenda kumzingua” Alisema dada huyo aliomba jina lake lihifadhiwe.
Dada huyo aliendelea kufunguka mengi kuhusu sakata hilo
“
Unajua sisi tunafanya biashara zetu hivyo kuna siku Shillole alikuja na
kusema amekwama kipesa hivyo tumuazime pesa na tukafanya hivyo lakini
cha kushangaza mwezi wa sita huu hataki kurudisha na amekuwa akitukwepa
mara kwa mara hivyo majirani ndio wakatushtua kuwa anataka kuhama kwa
staili ya kutoroka na deni letu ndipo tulipoenda wanawake wanne na
kumshushia kipigo” Alisema dada huyo
Baada ya taarifa
hizo Shilole alitafutwa kupita simu yake ya mkononi pamoja na kupita
kwenye makoloni yake hakuweza kupatikani isipokuwa majirani mbalimbali
walikiri kutokea kwa tukio hilo la kufedhehesha kwa msanii huyo.
0 comments: