MTU ASIYEJULIKANA AGAWA FEDHA KWA WATU JIJINI DAR....!!
Bajaji wakiwa kwenye foleni kuwekewa mafuta na mtu ambaye hakutaka kujitambulisha
Mwanaume mmoja, ambaye amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili,
amekuwa akigawa fedha za bure kwa watu mbalimbali jijini Dar.
Kijana huyo wa makamo, ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye
radio mbalimbali, aliwalipia bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili, wodi ya wanawake.
Akizungumza na mwandishi wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili,
Subira Juma alisema kijana huyo alikuja hospitali na kuuliza wangapi
wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na kisha kuondoka zake bila
kujitambulisha.
‘Kwa kweli hata mimi sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi
kuona mtu akitoa hela bila kujuana, na kisha kuondoka bila kusema
lolote’ alisema Subira.
Wakati huo huo, wasafiri wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao
wametajwa kunufaika na mgao huo, ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara
kadhaa na mtu huyo.
Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha
madereva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya
usafiri.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: