VIFO VYA WASANII... DOKII: MUNGU ANATUADHIBU KWA MABAYA YETU...!!
MWIGIZAJI Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ameibuka na kusema kuwa vifo
vya wasanii vimetokea kutokana na kujisahau hivyo Mungu ameamua
kuwaadhibu. Akichonga
na paparazi wetu katika Viwanja vya Leaders Club, Juni 5, mwaka huu
ambapo mwili wa Mangwea ulikuwa ukiagwa, Dokii alisema matukio ya vifo
vya wasanii mbalimbali yaliyotokea miaka miwili mfululizo ni pigo kubwa
kwani wengi ni vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kitu ambacho anakiona
ni ishara kuwa Mungu anataka kujidhihirisha kwa wasanii.

“Wasanii tulijisahau sana na kuona Mungu hayupo kwani kipindi bado hatujatoka na tunatafuta kutoka kisanaa, tulikuwa tunamuomba kila wakati lakini baada ya kutoka na kuwa mastaa tumemsahau kabisa.
“Hatukumbuki kwenda ibadani tunabaki kuendekeza starehe za dunia tu, hivyo tubadilike kwani Mungu ameanza kujionesha kwetu kwamba yupo,” alisema Dokii.

Dokii umenena, ila siku hizi uko wapi hatukuoni katika nynaja za kawaida, za kuigiza, kuimba na nyingine. Jitokeze ulielimisha sana enzi hizo, au nielekeze unapatikana katika nyanja zipi?
ReplyDeleteItakuwa vema tuwasiliane mtani