PICHA KADHAA ZA AJALI YA NDEGE YA KENYA AIRWAYS ILIYOTOKEA JANA JNIA


Dar es salaam imekua ikipokea mvua kubwa sana kwenye siku hizi za karibuni ambayo imehusika sana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa watu kuonyesha jinsi madimbwi yalivyotawala hata kwenye sehemu ambazo hazikutarajiwa barabarani.
Ukubwa wa hizi mvua ulisababisha ukungu mkubwa sana April 11 2014 mchana wakati ndege ya shirika la Kenya na abiria 49 ikiwa inatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam ikitokea Kenya.
Marubani walipata tabu wakati wa kutua hivyo ikatua kwa kishindo kilichopelekea ishindwe kutua kwenye barabara kama inavyotakiwa na badala yake ikaingia mpaka kwenye majani.
Screen Shot 2014-04-12 at 4.29.25 AMPolisi ilipozungumza na Radio One, imesema ajali hiyo ilisababisha kusitishwa kwa safari zote za ndege kuondoka na kutua huku abiria waliokuwemo ndani ya hii wakishushwa kwa dharura kama moja ya hizi picha inavyoonyesha hapo chini mwisho.
Sehemu ya injini ya upande wa kulia ya ndege hii iliyokua na Wafanyakazi saba ndani yake, imeharibika kutokana na kukita chini kwa kishindo wakati wa kutua.
Screen Shot 2014-04-12 at 4.29.39 AMHakuna yeyote aliepoteza maisha isipokua kuna taarifa chache za waliopata majeraha kidogo kwenye ngazi wakati wakishuka kwa dharura kama inavyoonekana kwenye picha ya mwisho chini.
Screen Shot 2014-04-12 at 4.29.49 AM
Screen Shot 2014-04-12 at 4.29.06 AM
Screen Shot 2014-04-12 at 4.29.00 AM
Screen Shot 2014-04-12 at 4.28.53 AM
Screen Shot 2014-04-12 at 4.28.32 AM
Screen Shot 2014-04-12 at 4.28.22 AM
Screen Shot 2014-04-12 at 6.24.25 AM
Screen Shot 2014-04-12 at 5.51.54 AMSource:Millaradayo
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: