KELVIN YONDANI APOTEA YANGA AKIWA SAFARINI KUELEKEA ARUSHA


Beki Kelvin Yondani hajulikani alipo, uongozi haujui na hata benchi la ufundi halitaki kulizungumzia suala Lake. Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa amesema hajui lolote kuhusiana na beki huyo na asingependa kuzungumzia.

“Sina taarifa yoyote kuhusiana na na Yondani,” alisema.

Lakini alipoulizwa bosi wake, Hans ven der Pluijm, naye alisema anachofanya ni kufanya wachezaji waliopo.

“Sasa nisingependa kumzungumzia Yondani, waliopo ndiyo ninafanya nao kazi na nguvu tunaelekeza katika mechi zilizobaki na tunataka kushinda zote,” alisema.

Viongozi wamekuwa wakikwepa kulizungumzia, lakini Yondani inaelezwa aliondoka mara tu baada ya mechi ya Mgambo ambayo Yanga ililala kwa mabao 2-1 mjini Tanga.

Rafiki wa karibu wa Yondani, amesema kwamba, beki huyo alikasirishwa na kuvishwa lawama alizoona hazikuwa na msingi, kwamba alihujumu kwa kuwa alisababisha penalty iliyozaa bao la pili.

“Unajua yeye ni beki, kosa linaweza kutokea na anaona anaonewa bila sababu za msingi na mbaya kuna baadhi ya viongozi wanaonekana kuungana na wale wasiojua mpira na kusisitiza alisababisha penalty kwa makusudi.

“Sasa hali hiyo imemuudhi na ukizingatia alicheza kwa nguvu sana, alijituma sana siku ile kwa kuwa anajua umuhimu wa ubingwa,” alisema rafiki yake huyo wa karibu bila ya kusema Yondani amejijimbia wapi.

Kabla ya kujiunga na Yanga, wakati huo akiwa Simba, Yondani alikimbilia kwao Mwanza na kujichimbia chanzo likiwa suala la lawama na kushutumiwa kuwa aliifungisha Simba makusudi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: