MTU WA AJABU ANAYEKULA MAWE NA MATOFALI KAMA MLO WAKE WA KILA SIKUMama yake  huwa anamuandalia kuku kama chakula cha siku lakini anakataa na kutaka apewe vipande vya matofali.
Kwa siku moja anakula vipande kadhaa vya matofali ambapo kwa makadirio huwa anakula kilo 3 kila siku.
Fundi huyo wa kujenga nyumba Pakkirappa Hunagundi anasema kwamba ameanza kula vitu kama hivyo tangu akiwa na miaka 10 na anaweza kukosa chakula lakini hawezi kukosa kula vipande vya matofali.
Akiwa anapata chakula chake hicho akipendacho(matofali) huwa anahitaji kikombe cha maji tu ili kushushia na mwenyewe anasisitiza kwamba hajisikii tofauti kabisa.
Mkazi huyo wa kijiji cha Karnataka nchini India anasema anataka kuzunguka India nzima akionyesha watu uwezo wake huo na kujipatia pesa kwa kuonyesha maajabu hayo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: