TANZANIA TUNAHITAJI RAIS MWENYE U DIKTETA KAMA KAGAME AJE KUBADILISHA MINDSET TUPATE MAENDELEO


Pamoja na propaganda niite za kitoto zinazoendeshwa na viongozi wa Tanzania pamoja na Baadhi ya watanzania dhidi ya Rais Paul kagame wa Rwanda kwa mtizamo wangu anaendelea kuwa Rais Bora barani Africa.

Ni rais pekee africa anaye weka mbele maslahi ya nchi yake kuliko kitu chochote. Kutokana na hiyo nia ya dhati amefanikiwa kwa kiasi fulani kupunguza saratani ya ukabila ndani ya Rwanda ndani ya miaka 20 tu. Si katika kuondoa ukabila tuu bali amefanikiwa kuboresha elimu na utoaji wa huduma za jamii hasa afya kwa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na nchi yeyote ya Africa. Kwa aliyebahatika kwenda Rwanda kabla ya Kagame atakubaliana na mimi jinsi rais kagame alivyo fanikiwa kwenye miundo mbinu, barabara , njia za mawasiliano etc.

Kuna wanao sema mafanikio hayo yameletwa na pesa zinazopatikana kutokana na uporaji wa madini Congo, Je ni nchi gani yenye kiongozi mwenye akili na commited kuleta maendeleo nchini kwake na wananchi wake haipori utajiri toka nchi nyingine?? Kwani marekani ilienda Iraq kuwasaidia wa Iraq?? ama waingereza na wafaransa walienda afganstan kuwasaidia wale waarabu???Mnajua wanawake na watoto wangapi wanakufa majeshi ya marekani yanapokuwa yanaenda kutafuta resources kwenye nchi nyingine??? Kwani hii mikataba mibovu tunayo lalamikia kila siku ya madini na makampuni , serikari za nchi yanako toka makampuni haya hawajui tunaibiwa?? Ama mnadhani Obama alikuja Tanzania kwa sababu anatupenda sana Wa Tanzania?? Rais mwenye akili anaye wapenda wananchi wake na nchi yake will do whatever it takes to bring about prosperity to his/her country. Eti Tanzania tunaenda kupigana Congo kwaajili ya kuwasaidia...Nchi za kusini mwa jangwa la sahara hususan South africa, Msumbiji etc tulizo zisaidia kupata uhuru wa kweli zinatusaidia nini leo hii zaidi ya kutushukuru tuu???


Tanzania inahitaji Rais mwenye u dikteta kama kagame aje kubadilisha mindset za watanzania kama tunataka maendeleo ya kweli vinginevyo hizi ngonjera tunazoimba kila siku hazita tupeleka kokote...Mtu yeyote anaye jaribu kuvuruga kilichojengwa anawekwa za kichwa kama yule generali aliyeuwawa hivi majuzi...Kiongozi yeyote mwenye vision anafanya hivyo kwa mvuruga nchi yeyote....Bongo kituko wanauwawa watu ki majungu majungu..mwangosi etl

WATANZANIA MAJUNGU NA WIVU WA KIKE HAUTA TUFIKISHA POPOTE
Source:Jamii Forums
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: