LINEX "ISSUE YA MIMI KUTOKA NA AGNESS MASOGANGE IMENISABABISHIA MATATIZO NA FAMILIA YANGU"Msanii kutoka Kigoma na memba wa kampuni ya Leka Dutigite Linex Sunday Mjeda ameendelea kutoa kilio chake juu ya uzushi ulioenezwa siku kadhaa zilizopita baada ya kupost picha mbalimbali akiwa na video vixen maarufu wa hapa bongo Agnes Gerald aka Masogange.

Baada ya picha hizo kusambaa Linex alikana habari zilizoandikwa na baadhi ya blogs kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mrembo huyo.
“ni kweli watu wa blog mnapush sana kazi zetu but nimesikitishwa na habari hii iliyoandikwa na blog kadhaa mtasababisha tutashindwa ata kukaa na Dada zetu au marafiki zetu Uliza b4 Hujaandika ujinga am single na sina haraka ya kua na mpenzi.” Aliandika Linex kwenye akaunti yake ya facebook.Kupitia Facebook jana mwimbaji huyo wa ‘Kimugina’ ameendelea kulalamika juu ya matokeo ya habari hizo za uzushi:
“Daaah Uzushi ulioenezwa na baadhi ya blog miyeyusho umesababisha Umenitofautisha na familia yangu ndugu jamaa na marafiki wish kama Mungu awafunue ndugu jamaa marafiki washabiki wangu waujue ukweli bado naendelea kupokea cm nyingi za maswali japo nilishaongea b4 kwamba sina mahusiano na Masogange daaaaah.”  

Credits:Bongo5
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: