TAZAMA JINSI MAGAZETI YA KITANZANIA YANAVYO TUCHANGANYA..JIONEE MWENYEWE HAPA
Huku amefumba macho! Hayo ni magazeti mawili ya jana yaliyokuja na takwimu mbili tofauti juu ya idadi ya tembo iliyobaki. Takwimu zenye kuzidi kutuchanganya ' Sisi watu wa Nchi ya Kusadikika'.
Maana, kwenye moja ya meza za magazeti, mwananchi baada ya kusoma taarifa hiyo nilimsikia akitamka kwa kukata tamaa; " Sasa hao 13 elfu waliobaki si watamalizika mwaka huu!"
Na ukweli unapatikana wapi?
Kwenye ukurasa wa pili wa The Guardian la leo inasomeka, kuwa ripoti inaeleza kuwa tembo 13,084 ndio waliobaki kwenye mfumo wa ekolojia kwenye hifadhi za Selous na Mikumi. Hapo hawajajumlishwa tembo wa Ruaha Rungwa na kwingineko.
Hata hivyo, idadi ya tembo inapungua kwa kasi kama tusipofanya jitihada za dhati kuukabili ujangili.
0 comments: