SHEHENA YA SAMAKI WALIOHARIBIKA YANASWA JIJINI DAR ES SALAAM..

Shehena ya samaki tani 22.5 kutoka nchini China wanaodaiwa kuharibika na kutokuwa salama kwa matumizi  ya binadamu wamekutwa katika eneo la Tabata Bima jijini dar es salaam huku baadhi ya samaki hao wakiwa tayari wamekwishaingizwa  sokoni kwa kuuzwa.

Baada ya kuwepo kwa fununu za uingizwaji wa samaki waodaiwa kuharibika kutoka nje ya nchi na  kuingia hapa nchini na kuatarisha maisha ya walaji,ITV  iliendelea kufuatilia tetesi hizo kwa kushirikiana na maafisa wa mamlaka ya chakula na dawa nchini-Tfda...

Lengo  la  ufuatiliaji  huo lilikuwa  ni kuwabaini wahusika wa samaki hao ambapo kwa eneo la tabata bima jijini dar es salaam kontena mbili zilikutwa zikitumika kuhifadhia samaki wa aina tofauti ..
Katika kontena ya kwanza inayomilikwa na kampuni ya SAIS Boutique inadaiwa iliingiza samaki aina ya vibua  tani 22.5 kutoa china  julai 2013 na kwa bahati mbaya samaki hao wamedaiwa kuharibika licha ya kuwa walishaanza kuuzwa sokoni tangu walipofika.

Afisa uhusiano wa mamlaka ya chakula na dawa nchini -Tfda Bi Gaudencia Simwanza,ameeleza kusikitishwa kwa uwepo wa samaki hao waliharibika katika kontena hiyo huku akiongeza kuwa kontena nyingine mali ya kampuni ya  Amasa Fish Traders iliyokuwa na samaki tani 27 aina ya vibua na kolekole kutoka nchini Yemen lazima ichunguzwe pia ili kubaini usalama wa samaki hao.

Mmiliki wa kontena iliyokutwa na samaki zilizoharibika Bwana Sadick Maporo,alikiri samaki wake kuharibika lakini akadai kuwa samaki hao waliharibika baada ya kufika hapa nchini kutokana na kukatikakatika kwa umeme.

Mamlaka ya chakula na dawa tfda wamedai hawajatoa idhini ya samaki hao kuhifadhiwa katika kontena hizo huku barua iliyoonyeshwa na mmiliki wa kontena hiyo haikuonyesha taarifa ya Tfda kama walikagua samaki hao walipofikishwa hapa nchini jambo linalotia shaka
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: