MBAKAJI ACHANGANYIKIWA BAADA YA KUAMBIWA KUWA MWANAMKE ALIYEMBAKA NI MWATHIRIKA WA VIRUSI VYA UKIMWI...!!

Mbakaji ambaye alifungwa jana anasubiria vipimo kubaini kama ameathirika na virusi vya ukimwi kutoka kwa muathirika aliye mbaka.
Richard Thomas, mwenye umri wa miaka 27, alianguka chini pale polisi walipomtaarifu kuhusu hali ya afya ya mwanamke huyo na anasubiria kusikia kama ameathirika na virusi hivyo visivyotibika. 
 
Thomas, mkazi wa Leigh huko Greater Manchester, alimfahamu mwanamke huyo na alijua kwamba ana ugonjwa mwingine lakini hakuwa akijua kuhusu virusi vya ukimwi. Mahakama ilielezwa alishitushwa pale alipotakiwa kupelekwa hospitali, Mahakama Kuu ya Liverpool ilielezwa.

Alijipeleka nyumbani kwake katikati ya usiku na mwanamke huyo akazinduka usingizini na kukuta Thomas akimbaka.

"Alitulia na hakuna aliyemwongelesha mwenzake. Alipangisha kaptula yake na kuondoka," alisema mwendesha mashitaka Harry Pepper.

"Alikamatwa na kuhojiwa na alisema alikuwa amelewa kupita kiasi, kutumia cocaine na kurukwa akili na hakuweza kukumbuka tukio hilo," aliongeza.

Wakili wake, Virginia Hayton, alisema kwamba bado hawezi kukumbuka shambulio hilo lakini alipoelezwa kuhusiana na hilo alisema kwamba mwanamke huyo 'hawezi kusema uongo, anaeleza ukweli. Kama anasema nimefanya hivyo, basi nimefanya'.

Akimfunga Thomas miaka mitano na miezi minne jela Jaji Mark Brown alisema kwamba amefanya 'kosa hili lisilopendeza' wakati mwanamke huyo akiwa amelala fofofo, akiwa amemeza vidonge vya usingizi, na ilimwacha akiwa mwenye mateso na wasiwasi.

Pia alimwamuru Thomas kusaini Rejista ya Wahalifu wa Kujamiiana kwa maisha. Thomas alipatikana na hatia ya kumbaka mwanamke huyo Julai 20 mwaka huu.

Hayton alisema kwamba Thomas, ambaye hapo kabla alishawahi kutiwa hatiani lakini si kwa makosa ya ubakaji, 'katili' na 'hawezi kuelewa kwanini alifanya vile na inamsumbua mno'.

Alisema kwamba alianza kutumia bangi akiwa na umri wa miaka tisa, kunywa pombe kupita kiasi akiwa na umri wa miaka 11, kutopea dawa za kulevya hadi kufikia kurukwa akili na cocaine akiwa na umri wa miaka 13 na aliwekwa chini ya uangalizi maalumu mwaka uliofuata.

Amekuwa akijaribu kuwasiliana na familia yake lakini hawataki kufanya chochote kumsaidia na sasa atakuwa mbali na mpenzi wake na binti yao mdogo na mabinti zake wengine wawili wakubwa aliowapa katika mahusiano yake ya awali.

Hayton aliieleza mahakama hiyo kwamba Thomas hawezi kupata majibu ya vipimo vyake vya virusi vya ukimwi hadi Ijumaa na amekuwa na hofu kubwa ya matokeo hayo.

"Ni kosa lake mwenyewe, kama asingefanya kosa hili asingejiweka mwenyewe mahali hapa."
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: