HAYA NI MAMBO 10 YAKUZINGATIA KATIKA MAPENZI

Watu wengi wamekuwa wakiyachukulia mapenzi kama kitu cha zawadi, ambacho mhusika hatakiwi kutazama ubora wake, kitu ambacho si sahihi.

Kwenye mapenzi kuna mambo kumi ya msingi ambayo yanataka umakini mkubwa katika kuyatenda, la sivyo madhara yanaweza kuwa makubwa. Mambo

hayo ni kama ifuatavyo:

1. KUCHAGUA- Tunapokuwa na hisia za mapenzi lazima umakini uwepo kwenye kuchagua. Ifahamike kuwa katika ulimwengu huu tunaoishi tuna wanaume na wanawake wengi hivyo jukumu letu kubwa litakuwa ni kuchagua mmoja wa kutufaa, kwa kuangalia kama ana sifa tunazohitaji.

2. KUKUBALI- Watu wengi siku hizi wamekuwa wepesi mno kukubali kutii hisia zao. Utakuta mtu anashawishika kimapenzi mpaka anachanganyikiwa kisa katumiwa ujumbe kwenye facebook au amepigiwa simu na kusikia sauti nzuri. Mapenzi ya kweli hayataki tabia hiyo, lazima tuwe makini tusikubali kujiingiza kwenye mapenzi kwa pupa.

3. KUJITAMBULISHA- Nyakati hizi wapenzi wamekuwa wepesi mno kuutambulisha uhusiano wao kwenye jamii. Utakuta msichana amefahamiana na mvulana wiki moja iliyopita, cha ajabu atawaambia watu wote: “Mimi mchumba wangu ni fulani.”

Tabia hii inaonesha mtu si makini, kwani kwenye mapenzi kuna suala la kujiridhisha kwanza na chaguo, kabla hujamtambulisha mwenza wako, vinginevyo utatambulisha wanawake wengi kwenu hadi wazazi watakupuuza.

4. KUBADILI DINI- Licha ya kwamba haikatazwi mtu kubadili dini ili aolewe/aoe, lakini ni vyema kila mtu akafahamu kuwa suala hili linahitaji umakini sana kulifikia.

Upo ushahidi wa kutosha unaoonesha kuwa mtazamo wa familia hutofautiana sana pale mmoja wao anapoamua kubadili dini kwa lengo la kuoa au kuolewa.

Hii ina maana kwamba kabla ya kufikia hatua hiyo ni vyema mtu akafikiria kwa kina, asije akabadili dini leo halafu kesho akajikuta mume aliyekuwa anampapatikia si lolote kwake. Hali hii itakuwa imemletea matatizo makubwa kwenye familia yake na hata ndani ya nafsi yake mwenyewe.

5. KUZAA- Kuna watu si makini kabisa kwenye suala la kuamua azae na nani na kwa faida gani? Utakuta baba ana watoto kumi, lakini kila mmoja na mama yake. Hili si jambo jema, hata kama umempenda mwanaume fulani jiulize kwanza ni sahihi kwako kuzaa naye?

6. KUGAWA MALI- Wapenzi wengi wamejikuta kwenye majuto makubwa baada ya kuamua kwa pupa kuwagawia sehemu ya mali wapenzi wao.

Utasikia mwanzo tu wa uhusiano jamaa anamwambia mpenzi wake: “Nimeamua kiwanja cha Mbezi niandike jina lako na duka la Mchungwani litakuwa lako. Haya ni makosa.

7. KUAMINI-Wapenzi msiwe wepesi sana kuwaamini wenzenu, jambo la imani linahitaji muda kulifikia. Isitokee kwa haraka ukamuamini mpenzi wako na kuweka wazi kila kitu zikiwemo namba za siri za benki. Umakini unahitajika sana.

8. KUELEZA UKWELI- Ingawa mapenzi yanataka ukweli lakini kuuendea ni jambo linalohitaji umakini. Haitakuwa busara kumwambia mpenzi wako kuwa uliwahi kubakwa na watu kumi miaka miwili iliyopita, au ulishafungwa kwa ujambazi. Yote hayo lazima yatazamwe kwanza ili kuchuja faida na hasara zake kwa mwenzako.

9. KURUDIANA- Katika mapenzi kuna wakati mnaweza kutengana kwa sababu mbalimbali. Hali hii inapotokea wahusika wasirudiane bila kujichunguza na kuwa na maamuzi ya msingi, vinginevyo wanaweza kujikuta wakijutia uamuzi wa kurudia ‘matapishi’ yao.

10. KUACHANA- Mnapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na ikatokea hali ya kuhitilafiana katika hili na lile, haifai kukimbilia kuachana


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: