CAG ADAI KWAMBA MAGUFULI SIYO FISADI.....ATOA UFAFANUZI WA KINA KUHUSU ZILE BIL. 252
MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema taarifa ya Sh bilioni 252 zilizokuwa zimeoneshwa katika taarifa ya Wizara ya Ujenzi, zilihamishwa kwenda Wakala wa Barabara (Tanroads) kulipia madeni ya wakandarasi na kwamba hapakuwa na ufisadi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Utouh alisema vyombo vya
habari viliripoti suala hilo tofauti, baada ya Kamati ya Hesabu za
Serikali (PAC) kukutana na wizara na kuhoji juu ya matumizi ya fedha
hizo.
Utouh
alisema baada ya PAC na Kamati ya Kudumu ya Serikali za Mitaa (LAAC)
kupitia ripoti ya Wizara ya Ujenzi, kumejitokeza upotoshaji wa taarifa
kuhusu hesabu za wizara hiyo na taarifa zisizo sahihi, zikidai kulikuwa
na ufisadi.
Alisema
fedha hizo zimeoneshwa kwenye taarifa ya hesabu za Wizara hiyo, kama
vile ni miradi mipya ya mwaka 2011/2012 tofauti na uhalisia wake.
Utouh
alisema uhalisia wa fedha hizo ni kuwa mara baada ya kupokewa na Wizara
ya Ujenzi kutoka Hazina, zilihamishwa kwenda Tanroads kulipia madeni ya
wakandarasi wa miradi ya barabara, iliyotekelezwa na wahandisi
washauri, ambao walikuwa hawajalipwa kwenye mwaka wa fedha 2010/2011.
“Fedha
hizi zilijumuishwa kimakosa kwenye hesabu za Wizara kama matumizi ya
akaunti ya maendeleo, hivyo kuongeza matumizi ya Wizara kimakosa kwa
kiasi hicho.
Kihasibu fedha hizo zilipaswa kuoneshwa kwenye hesabu za mtumiaji halisi wa fedha ambaye ni Tanroads na siyo Wizara hiyo,” alisema Utouh.
Kihasibu fedha hizo zilipaswa kuoneshwa kwenye hesabu za mtumiaji halisi wa fedha ambaye ni Tanroads na siyo Wizara hiyo,” alisema Utouh.
Alisema
kutokana na hali hiyo, hesabu za wizara hazikuwa sahihi, kutokana na
uwepo wa ongezeko hilo kubwa la fedha na hivyo kusababisha kupewa hati
ya ukaguzi yenye mashaka.
“Hivyo
katika kujadili hesabu za Wizara ya Ujenzi hakukuwepo na tuhuma zozote
za ufisadi, ila Kamati ya PAC ilimtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali kuihakikishia matumizi ya fedha hizo, jambo ambalo
tumejiridhisha nalo kwa ushahidi wa namna mlolongo wake ulivyo hadi
zilipotumika” aliongeza Utouh.
Aidha,
alisema mbali na dosari hiyo ya kihasibu, Wizara ya Ujenzi inafanya
kazi nzuri ya kusimamia na kujenga barabara katika kona zote za nchi,
hivyo viongozi wake wanapaswa kupongezwa kwa kazi hiyo wanayoifanya huku
akiwataka kuwa na moyo wa kuchapa kazi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya
taifa.
Katika
hatua nyingine, Utouh alimpongeza Spika wa Bunge Anne Makinda kwa
uamuzi wake wa kupanga upya Kamati za Kudumu ya Hesabu za Serikali Kuu
(PAC), kwa madai kuwa utasaidia kuleta ufanisi na tija katika utendaji
kazi wa kamati hiyo.
Alisema
uamuzi wa Spika kuipanga upya PAC na kuwa na vyombo viwili PAC 1,
itakayokuwa ikishughulikia taarifa za Hesabu za Serikali Kuu, idara
zinazojitegemea na taasisi zingine za Serikali chini ya Mwenyekiti wake
Zitto Kabwe na PAC 11, itakayokuwa ikishughulikia hesabu za Mashirika ya
Umma chini ya uenyekiti wa Deo Filikunjombe, kutasaidia kuleta ufanisi
mkubwa katika ufuatiliaji.
-Habarileo
-Habarileo
0 comments: