SERIKALI YA KENYA YAZIFUNGA SHULE ZOTE ZA MSINGI NCHINI HUMO BAADA YA WALIMU KUGOMA KUINGIA MADARASANI KUFUNDISHA.


SERIKALI nchini Kenya imetangaza kuzifunga shule zote za msingi za umma kufuatia kuendelea kwa mgomo wa walimu mfululizo ulioingia wiki ya nne hivi sasa.

Taarifa zinasema Waziri wa elimu wa nchi hiyo, Profesa Jacob Kaimenyi ametangaza kuzifunga shule hizo, huku akisema kuwa zinafungwa kwa muda usiojulikana. Hata hivyo waziri huyo amewashutumu walimu akisema kitendo walichokifanya si cha kiungwana kwani mgomo wao ulikuwa kinyume na sheria.

Zaidi ya walimu 240,000 nchini humo wamesusia kutoa mafunzo kwa wanafunzi kwa zaidi ya mwezi sasa wakidai nyongeza ya asilimia 500 ya mishahara waliyoahidiwa na Serikali mwaka wa 2007. 

 

WALIMU HAO PIA WANATAKA KUONGEZEWA MARUPURUPU YA USAFIRI, NYUMBA PAMOJA NA MATIBABU. SERIKALI IMESEMA KUWA WAZAZI WATAARIFIWA JUU YA SIKU YA KUFUNGULIWA TENA KWA SHULE HIZO.

WAZIRI HUYO WA ELIMU PROF. KAIMENYO ALISEMA KUWA WIZARA YAKE ITAFANYA MIPANGO MAALUMU KWA AJILI YA WANAFUNZI WA DARASA LA NANE WANAOTARAJIWA KUFANYA MTIHANI WAO WA KITAIFA CHINI YA MIEZI MINNE IJAYO

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: