RAIS OMARI AL BASHIR WA SUDANI ATOROKA NIGERIA BAADA MBINU ZA KUMKAMATA KUVUJA



Rais  Omari Al Bashir  wa  Sudan  jana  alilazimika  kutoroka  nchini    Nigeria  baada  ya  mikakati  ya  kumkamata  kuvuja..

Rais Bashir aliyekuwa  anahudhuria mkutano wa viongozi wa serikali za nchi za Muungano wa Afrika AU, kuhusu afya mjini Abuja amelezimika  kuukatisha  mkutano  huo na kutoroka  nchini  humo  jana  Jumatatu  kwa  hofu  ya  kukamatwa


Rais  huyo  ameondoka  nchini  Nigeria  ikiwa  ni  chini  ya  masaa  24  tangu  awasili  Nigeria 


Makundi ya kutetea haki za kibinadam yameishutumu  vikali  serikali ya Nigeria, kwa kumualika rais wa Sudan, Omal al-Bashir, nchini Nigeria na siku ya jumapili walilitaka jeshi la nchi hiyo kumkamata rais huyo wa Sudan  kabla  hajaondoka.


Makundi hayo ya kutetea haki za kibinadam yamesema kuwa, ziara hiyo ni dharau  kwa wahanga wa mzozo huo unaoendelea katika eneo la Darfur.
  

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa rais huyo kwa Sudan kwa tuhumu za kuhusika na mauaji ya halaiki. 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: