MKASA:HAUSIGELI ANASWA AKIUZA DUKA LA MADAWA


KATIKA HALI ISIYOKUWA YA KAWAIDA HAUSIGELI AITWAYE FURAHA AMENASWA AKIWA KATIKA DUKA LA MADAWA ANAUZA BAADA YA KUPOKEA MALALAMIKO KUTOKA KWA WATU MBALIMBALI WAKIDAI MHUSIKA MWENYEWE AKIWA KATIKA KAZI NYINGINE TOFAUTI NA DUKA HILO.

TUKIO HILO LINADAIWA KUFANYIKA KWA MUDA MREFU KATIKA DUKA HILO LILILOPO GOROKA, TOANGOMA, KONGOWE, TEMEKE NJE KIDOGO YA JIJI LA DAR.


Akiwa katika famasi akisubiri wateja.

Baada taarifa hizo, ulianza utafiti ambapo iligundulika kuwa mmiliki wa duka hilo anatambulika kwa jina la mama Atu.

Ikadaiwa kuwa mmiliki huyo ana tabia ya kumuachia duka hilo hausigeli wake aitwaye Furaha ili auze dawa kwa kubahatisha na mara kadhaa wagonjwa hupewa dozi ndivyo sivyo.

“Kuna mwenzetu alikuwa akiugua ugonjwa mwingine, alipofika pale aliandikiwa dawa za malaria, hali yake ikawa mbaya hadi akakimbizwa hospitalini kulazwa, tulipomuonya mmiliki hakutusikia,” alisema mmoja wa watu wanaoijua ishu hiyo kiundani.

Ili kupata ushahidi kamili, Mtu mmoja ilijifanya mgonjwa na kwenda kwenye famasi hiyo kuomba ushauri wa matibabu.



Akimsikiliza mteja.

Hausigeli huyo alimtajia dawa za typhoid lakini shushushu wetu alimkwepesha na kumuomba chloroquine ambapo hausigeli huyo alikubali na kutaka kumpa bila wasiwasi.

Baada ya kushuhudia hayo alifatwa mwenyekiti wa mtaa huo, Issa Shomari kupitia mjumbe wake na kufika katika famasi hiyo kujionea hali halisi ambapo kama ilivyokuwa mwanzo hausigeli huyo alikuwa tayari kutoa huduma.

Baada ya kikosi kazi kujitambulisha na kumhoji, alikiri kuwa yeye ni mtumishi wa ndani, ana miaka 16, elimu ya darasa la saba, mwenyeji wa Iringa, huwa anaachiwa auze na mwajiri wake huku akifunguka kuwa hutoa dawa za malaria na magonjwa anayoyafahamu.

Akizungumza kwa mshtuko baada ya kujionea hali halisi, mwenyekiti huyo wa mtaa alisema kuwa atahakikisha anawasiliana na kamati ya afya ya Wilaya ya Temeke, Dar ili kuziondoa famasi kama hizo mtaani kwake.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: