BAADA YA JESHI LA POLISI KUPIGA MARUFUKU KIKUNDI CHA ULINZI CHA CHADEMA 'RED BRIGADE', CCM NAYO YAANZISHA CHA KWAO KINACHOITWA 'GREEN GUARD'...!!


VIJANA WA ULINZI WA CCM, WANAOJULIKANA KAMA CHIPUKIZI AU ‘GREEN GUARD’ WAKIWA KATIKA MAZOEZI KATIKA SHUGHULI ZA CHAMA. PICHA NA MAKTABA 


Wakati Rais Jakaya Kikwete akiponda mpango wa Chadema kuanzisha kambi za mafunzo kwa ajili ya mafunzo ya ulinzi, imeelezwa kuwa Chama Cha Mapinduzi nacho kimekuwa kikiendesha mafunzo ya ukakamavu kwa vijana wake.

Hata hivyo alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu kuendesha mafunzo hayo, Naibu Katibu wa CCM, Mwigulu Nchemba alisita kuzungumza na kumtaka mwandishi aangalie ukurasa wake wa Facebook ambako amefafanua.

Katika ukurasa huo, Mwigulu amekosoa Rasimu ya Katiba Mpya akisema muundo wake utaleta utata wa usalama.  Mwigulu ametaja ibara ya 223(1) inayozungumzia uanzishwaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ),  litakalokuwa na mamlaka ya kusimamia ulinzi na usalama,  “Ibara ya 232(1) inasema bila kuathiri masharti ya Katiba hii, nchi Washarika wa Muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi na usalama .... katika maeneo yao.

 Ametaja pia ibara ya 227(1) inayoeleza uundwaji wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano na ibara ya 232 inayozungumzia vikosi vya washirika kuhusika na ulinzi wa watu wao na ibara ya 233 (1) inayozungumzia Idara ya Usalama wa Taifa wa Jamhuri ya Muungano.

 “Suala la usalama ni nyeti muundo huu utategemea tu mazingira na busara ya viongozi. Vinginevyo ni rahisi vikosi vya Muungano kupigana na vya nchi washirika kufuatia maelekezo ya viongozi wao siku wakitokea sio wataifa,”


Akifunga kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Dar es Salaam juzi, Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM pia alikosoa kitendo cha Chadema kususia mkutano. “Sasa hawa kweli wanapenda amani yetu wakati hawapendi tuzungumze,wanataka watu wauane,wapigane,” alisema.

  Mbali na Rais Kikwete,Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, SSP Advera Senso limekionya Chadema kuhusu mpango huo.   “Kitendo cha chama chochote cha siasa ikiwamo Chadema kuanzisha kikundi cha kujihami ni kinyume cha sheria za nchi na endapo watafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi na litachukua hatua kulingana na ushahidi utakaopatikana.

 “Jeshi la Polisi litamshughulikia mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria bila kujali wadhifa wake,” alisema Senso katika taarifa yake.

Hata hivyo,mtindo wa kuanzisha vikundi vya ulinzi kwa vyama vya siasa unaonekana kuzoeleka huku vyama vikubwa vikiwa na makundi kama vile Red Brigade ya Chadema,Green Guard ya CCM na Blue Guard ya CUF.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: