M TO THE P AWASHUKURU MASHABIKI KUFIKA SHOO YA JAYDEE


M To The P ambaye aliyekuwa swahiba wa msanii Albert Mangwea 'Ngwair' jana aliweza kuonyesha mapenzi yake kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Jaydee kwa kufika katika onyesho hilo lililofanyika Nyumbani Lough jijini Dar es Salaam.

M To The P ambaye pia na  yeye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya aliweza kufika mahali hapo na kupanda jukwaani baada ya kuitwa katika jukwaa hilo na msanii mwenzake Juma Nature kwa madhumuni ya kuwasalimu mashabiki waliofika hapo

M To The P aliweza kupata nafasi ya kuzungumza na mashabiki wake pamoja na kuwashukuru kwa msaada waliouonyesha kipindi alichokuwa anaumwa akiwa nchini Afrika Kusini, baada ya salamu hizo shoo iliendelea ambapo msanii Juma Nature aliweza kuwapagawisha mashabiki waliojazana mahali hapo huku wengine wakikosa sehemu ya kukaa na kusimama
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: