HII NDIO RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA NGWEA PINDI MWILI WAKE UTAKAPOFIKA...!!

Tuesday, June 4, 2013 | 3:37 PM

Wanakamati wa mazishi pamoja na wasanii akiwepo Profesa Jay, Lady Jaydee, Fid Q, Stamina, Juma Nature na wengine wengi wanaelekea uwanja wa ndege kutoka Viwanja vya Leaders tayari kuupokea mwili wa Mangweha.
-Mwili utawasili saa 8 mchana huu.
-Baada ya mwili kuwasili uwanja wa ndege, utapelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo utapokelewa na kuhifadhiwa.
-Baada ya kuhifadhi mwili, waombolezaji wataelekea Viwanja vya Leaders kwa maombolezo.


-Kesho saa 2 asubuhi mwili utakuwa Viwanja vya Leaders kwa ajili ya kuagwa mpaka saa 6 mchana.
-Saa 6 mchana mwili utasafirishwa kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya ratiba nyinginezo

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

1 comment:

  1. endeleni hivyo wasanii wa muziki wa bongo.....R...I....P...Ngwea

    ReplyDelete