UKWELI WNGU UMENIPONZA NAJUTA NIMETOKA NJIA KUU NA KUMWAMBIA MKE WANGU
Takriban wiki moja imepita tangu nilipofanya mazungumzo na mke wangu, nilidiriki kumweleza ukweli kuwa kwa kipindi kirefu nilikuwa natoka nje ya ndoa, na hivyo nikamwomba anisamehe na kuwa najutia nakumwahidi kuwa sintofanya hivyo tena kwani hakuna nilichokipata. Baada ya mazungumzo yetu alionyesha kuniunga mkono kwa kunionyesha upendo wa dhati na mimi pia hali kadhalika. Sasa kilichonichanganya namwona mke wangu kanichenjia hataki kuongea na mimi kila kitu anatuma mtoto, nimwulizapo kulikoni? kimya sijibiwi, kibaya zaidi hataki nimguse ukizingatia kuwa wanandoa ndiyo huwa njia yetu pekee ya kutatua na kuondoa tofauti zilizopo, hakuna amani Nifanye nini sasa wadau wa blogs ya chumba cha siri
0 comments: