HII NDIO IDADI YA TEMBO WALIO BAKI MBUGA YA SELUU


Meno ya tembo bado ni ishu kubwa na stori zake bado zinazidi kumiliki headlines kutokana na ukweli kuhusu wanyama hawa wanavyoshambuliwa na majangili mbalimbali,February 20 Meneja uhusiano wa hifadhi ya Seluu ametoa idadi kamili ya Tembo waliobaki.
February 20 2014 mara baada ya kukabidhiwa zaidi ya Milioni 42.5 kutoka hotel zilizopo Seluu Mr Benson Kibonde ambaye ndiye Meneja uhusiano wa mbuga ya Seluu amesema>> ‘Hali  hii si nzuri kabisa licha ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali’
Ingawa mpaka sasa haijatoka idadi kamili ya mbuga zingine jumla ya tembo waliuwawa lakini kwa mbuga ya Seluu peke yake imebakisha tembo 13,000 tu kutoka 70,000 waliokuwepo mwaka 1990 kwa mujibu wa Mr Kibonde.

Miongoni mwa sababu alizozi-amplify Mr Kibonde ni kuhusu majangili hao ambao amesema ujangili ni tatizo kubwa ambalo unafanywa na watu wenye fedha nyingi na wana mtandao wa kimataifa hali inayosababisha kazi hiyo kuwa ngumu.
Bado mbuga zetu za Tanzania zina changamoto nyingi ambazo miongoni mwa alizozieleza Mr.Kibonde ni pamoja na kufanya kazi kwenye mazingira magumu,mafuta ya magari kutojitosheleza, chakula na vitendea kazi vingine kukosekana.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: