UTEUZI WA JUMA NKAMIA NI KUUA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI-MEENA

Akiongea na kituo cha CHANNEL TEN leo jumapili tarehe 19/01/2014,mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi ndugu Meena amelaani uteuzi wa Jumaa Nkamia kuongoza wizara inayosimamia vyombo vya habari,nanukuu,"Nkamia nimesoma naye,lakini kauli zake za hivi karibuni bungeni vinaonesha kuwa hapendi uhuru wa vyombo vya habari,kwa aliyofanya waziri aliyepita na kwa uteuzi wa Nkamia tutegemee kuminywa kabisa kwa vyombo vya habari".

Nilitegemea kuteuliwa kwa mtangazaji mkongwe Nkamia kungewafurahisha waandishi wa habari,lakini inaonekana sivyo.Je, ni kweli Nkamia hafai kuongoza wizara ya habari,au ni chuki binafsi za Meena kwa Nkamia.Nini mapungufu ya Nkamia mpaka akachukiwa kiasi hicho na Meena? Kama si Nkamia,nani anafaa kuongoza wizara husika?.
Source:Jamii Forums
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: