PENNY AAMUA KUFUNGUKA KUHUSU KUVUNJIKA MAPENZI YAO NA DIAMOND..HUU NDIO UKWELI NA NINI KINAENDELEA SASA


Mtangazaji na meneja wa vipindi wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mwingila aka VJ Penny, amesema kuwa yeye na mpenzi wake, staa wa ‘My Number One’, Diamond Platnumz, wamepeana nafasi ili kila mmoja kutafakari anachotaka maishani.

Kauli ya Penny kwenye mahojiano maalum na Bongo5 TV, inajibu maswali ya wengi kuhusiana na kama wawili hao wapo pamoja au wameachana baada ya Diamond na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu kurudiana tena. Katika interview hiyo, Penny ameongea pia kuanzia historia yake, namna alivyoingia kwenye utangazaji, alivyokutana na Diamond, mapenzi yao yalivyokuwa, alivyojisikia baada ya kuona picha za Wema na Diamond, maisha yake ya sasa na mipango yake ya mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu alivyojisikia baada ya kuona picha za Diamond akiwa na Wema, Penny amesema yeye pia alishangaa kama watu wengine walivyoshangaa kuziona.

“Mimi ni mtu ambaye utaniambia ‘fulani amefariki’ na sitakiamini mpaka nione kabisa huyu hapa amekufa,” amesema Penny. “Nilipoziona picha nilishtuka kidogo, kibinadamu nilikuwa ‘Ohh Mungu wangu kipi kinaendelea’. Lakini sijui.. Mungu wa ajabu sana, niliichukulia kwa uzito mdogo kadri nilivyoweza, ilipita tu kama ‘shaaa’.. na dakika inayofuata (Diamond) anasema ‘ohh ni movie’. Mimi nilikuwa kama nyie, amini usiamini ‘Ni movie okay vizuri, baby anafanya movie’. Kwa kawaida nilitakuwa kuipokea tofauti lakini ni kama nilishikwa na ganzi kwa muda, sikutaka kujiumiza. Kuna ‘buttom’ ambayo nikiruhusu iniumize nitaumia, nikiamua kitu kinipite na siwezi hata kujisumbua. Alirejea, maisha yakaendelea, nimekaa nasubiri movie hiyo.”

Penny amesema pamoja na yote hayo, maisha yaliendelea kama kawaida kati yao kama vile hakuna kilichotokea.

“Alirejea kutoka kwenye safari yake ya movie na tuliendelea kuwa pamoja kwasababu mimi nilikuwa nani kuhukumu tofauti? Hicho ndicho kitu nawaambia watu, sikuwepo hivyo kama anasema alikuwa anafanya movie nitamuamini kwasababu sikuwepo. Napenda kuona vitu mwenyewe, mimi ni mtu wa hivyo, nahukumu vitu pindi nionapo mwenyewe. Maisha yaliendelea, tuliendelea kuwa sisi. Nilikuwa na vitu vilivyokuwa vikizunguka kwenye mawazo yangu nje na ndani.. ‘hivi ndivyo natakiwa kuwa?’ Watu wanadhani nina moyo wa jiwe, nina moyo, nina akili, saa zingine inabidi nikae nifikirie, nini hiki, nini kile. Mambo yalikuwa sawa lakini tofauti kidogo kuzingatia ukweli kwamba sikujua nini cha kufikiria, sikujua nini cha kufanya na nilitakiwa kuchukua muda wangu kuhakikisha kuwa sifanyi kosa lolote. Na nilikuwa bado pembeni yake, bado nikimsupport chochote alichokuwa akikifanya iwe movie, nyimbo zake mpya au chochote, niliendelea kuwepo kwaajili yake kuwa girlfriend wake, rafiki yake wa dhati, mkono wake wa kulia.”

Hata hivyo Penny amesema ilifika wakati ambapo waliona bora ‘kupumzisha’ uhusiano wao kutokana na hali halisi ya mabadiliko yaliyokuwa yamejitokeza.

“Kama uhusiano wowote ulivyo, kuna mwanzo na mwisho na watu wanaachana kwa sababu nyingi. Nilihisi kwamba nahitaji kumpa nafasi, wote ni vijana na wakati mwingine tunahitaji nafasi kugundua vitu vipya, kuona kipi hasa unachokihitaji kwenye maisha. Unajua ukimruhusu ndege afanye vitu mbalimbali then atajua kama ‘mti huu ndio unanifaa, mti huu haunifai. Hivyo nilihisi kwamba wote tulihitaji hicho, tulihitaji ‘space’ hivyo nikampa nafasi na mimi nakuchukua nafasi. Huwa nawaambia watu kuwa vyovyote ilivyo, yeyote atakayekuwa naye, nipo pembeni yake nikimshangilia kwasababu ni kweli (Diamond) ni mtu mzuri ndani. Achana na watu wanavyomuona chizi chizi, sahau msanii unayemjua, ana roho nzuri na anajua anachokitaka. Ni ngumu kuacha iende.. kama ni rahisi kuacha iende basi hujampenda huyo mtu.”


Amesema kila anapoulizwa maswali ya ni nani kati yake na Diamond aliyemwacha mwenzake, hujibu hajui kwakuwa wamepeana tu nafasi ya kila mtu kufanya mambo yake na kuongeza kuwa bado wanaendelea kuwasiliana huku akiwa na furaha na chochote (Diamond) anachofanya.

Penny amesema japo ameendelea na maisha yake lakini bado anachukua muda kufikiria nini anachohitaji maishani na hadi sasa hajafikiria kuwa na mwanaume mwingine. “Bado, sio kwamba sitongozwi, wanaume wanakuja lakini najaribu … hakuna mwanaume mkamilifu, najaribu kutafuta mwanaume anayeweza kuwa mkamilifu kidogo najua yupo sehemu.”


Ameongeza kuwa anatamani kurejea katika maisha ya kawaida na kuwa na uhusiano na mwanaume asiye maarufu kwakuwa kuwa na uhusiano na mtu mwenye jina kulimfanya achunguzwe muda wote na kujikuta akikosa maisha ‘faragha’.

“Napenda kurejea kwenye maisha niliyokuwa nayo ‘it was much fun’, napenda maisha yangu ya faragha.”

Penny amesisitiza kuwa mwaka 2014 ameupanga kuwa mwaka wa kufanya kazi zaidi na anaamini utakuwa wa ushindi kwake.


“Nilijiambia mwenyewe siku ya January 1 kuwa ‘mwaka huu ni mwaka wa ushindi kwangu’ na naenda kushinda, vyovyote vile naenda kushinda, naenda kuweka nguvu yangu yote, kwahiyo kuna mengi yanakuja, mengi.”

Source:Bongo5.com
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: