KAGAME ANUSURIKA KIFO
RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amenusurika kifo baada ya msafara wake nchini Kenya kupata ajali na kusababisha watu wawili kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), imeelezwa kuwa ajali hiyo ilihusisha mojawapo ya magari ya msafara wake nchini Kenya, alipokuwa kwenye ziara za kikazi.
Hata hivyo, Rais Kagame hakujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi jana eneo la Limuru nchini Kenya. Dereva wa gari hilo alipoteza mwelekeo katika barabara kuu ya Nairobi-Limuru, hata hivyo gari hilo lilikuwa mbali na msafara wa rais huyo. Aidha majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa haraka hospitalini.
Rais Kagame alikuwa anarejea mjini Nairobi kutoka katika kongamano la Magavana wa Kenya mjini Naivasha katika Bonde la Ufa.
Kagame alialikwa kuhudhuria kongamano la Magavana nchini Kenya, kuhusu uongozi mzuri na utawala bora.
0 comments: