MCHUNGAJI GWAJIMA NDANI YA KASHFA NZITO, WASAIDIZI WAKE WAMPIGA MWANDISHI WA HABARI HADI KUTENGUA KIUNO
Mchungaji Josephat Gwajima na wasaaidizi wake wameingia kwenye kashfa nzito ya kumshambulia mwandishi wa habari Mkoani Tanga Ndugu Eliasi Mokiwa hadi kumtengua kiuno chake kisa kikiwa kuwapiga picha misukule wake aliodai kuwagomboa mikononi mwa wachawi wa Tanga.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na mwandishi wetu aliyekuwepo eneo ya tukio huko Mkoani Tanga ambako Gwajima na wafuasi wake waolikuwa wakifanya hudia misukule.
Akizungumzia tuki hilo mwandish huyo ambae anaripotia gazeti la Jibu la Maisha lakini ni mwanafunzi wa chuo cha Royal College ngazi ya Cheti kilichopo Mkoani humo alisema ilikuwa siku ya tarehe moja desemba 2013 saa kumi za jioni aliwa na mwandishi wa gazeti hili Mkoani Tanga Bwa Sadiki Amidu na wakiwa kwenye viwanja vya Tangamana wakati mchungaji huyo akitangaza kuwa kuna msukule amedondoka katikati ya watu.
Mwandishi huyo anasema alisogea na yeye ili kushuhudia msukule huyo pamoja na kumpiga picha lakini katika hali isiyotarajia baada ya kupiga picha moja alishtuka amepaishwa juu kumbe kuna msaidizi wa Gwajima ambae alimpiga mtama ulimpaisha kimo cha ng’ombe na kudondoke kiuno.
Mara baada ya kutua nchini mwandishi huyo anasema alisikia kitu flani kimelia kwenye kiuno chake kumbe nyonga ilikuwa imeshateguka ambapo wakati akigragara chini walikuwa wasaidiz wanne na walimbeba juu hadi nyuma ya jukwaa na kuanza kumsurubu, wakati huo Mchungaji Gwajima alikuwa anashuhudia mchezo mzima bila kutoa kauri yeyote.
Mwandishi huyo aliendelea kueleza “ Nilipigwa sana huku wakinisachi mifukoni na kunichukulia pesa yangu yote ambayo ilikuwa ni shilingi elfu tano ya nauli huku wengine wakiniuliza kama pesa nyingine nimeweka wapi lakini kiwajibu kuwa sina pesa nyingine na kuwaeleza mimi ni mwandishi wa habari hivyo wasinidhalilishe kiasi hicho lakini hawakutaka kusikia” Alisema Eliasi
Hata hivyo Eliasi aliendelea kusema kuwa “ Mwandishi mwezangu baada ya kuona vile alitimua mbio kuokoa maisha yake kwani walishashtukia kuwa tuko wawili hivyo huenda wangetukamata wote, baadae alikuwa mchungaji mmoja mwanamke ambae sikufahamu labda huenda alikuwa mke wa Gwajima kutokana na heshima waliyompa muda ule kwani wakiwa bado wananishambulia kwa ngumi za chembe na walipomuona mama huyo waliniacha haraka na kuganda” Alisema mwandishi huyo
Baada ya mama huyo kuuliza kosa langu nini wakamueleza kuwa kuwa mimi nimepiga picha misukule na nilikuwa navizia watu waliokaa uchi na kuwapiga pamoja na misukule yao, ambapo mama huyo aliamuru niachiwe huru lakini kama hizo picha za misukule zipo kwenye kamera yangu zifutwe halafu wanirusu na mama huyo aliangalia kwenye kamera na kukuta hamna picha yoyote ya aina hiyo.
Hata hivyo Eliasi aliendelea kusema “Nilivyoachiwa huku nikiwa nyang’anyang’a nilijisogeza kidogo kidoga hadi kituo kikuu cha Polisi na kutoa taarifa na wakampatia Jarada la Upelelezi PE namba 71 -2013 pamoja PF3 ambapo alikwenda kwenye Hospitali ya Jiji ambako walimpatia matibabu hadi siku iliyofuta ambapo alirudi na ile PF3 tena Polisi.
Aidha kutokana na mkutano huo kuwa isku ya mwisho kwenye viwanja hivyo na wakahitaji kuongeza siku za mkutano lakini walizuiwa kibari badara yake walihamishia mkutano huo kwenye viwanja vya Ridochi. Na baada ya siku mbili Polisi wakiwa na Deffender walikwenda kuvamia mkutano huo kwa lengo la kuwakamata wale wote walihusika na tukio la kumpiga na kujeruhi mwandishi huyo, lakini kwa bahati mbaya mwandishi huyo akiwa ameandamana na Askari hakuwata wale walimpiga hivyo na kufanya Polisi kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Baada ya taarifa hizo Maskani Bongo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga “RPC” Masawe ili kuzungumzia ishu hiyo ambapo alipatikana lakini kwa bahati mbaya akajibu kuwa yuko kwenye mafunzo Moshi hiyo tumtafute Kaimu wake ambae nae alipopigiwa simu simu hiyo iliita tu bila kupokelewa.
Misukule ya mchungaji Gwajima imekuwa na utata mkubwa sana kwenye jamii kutokana na wengi kuamini kuwa ni propaganda tu za kujizolea waumini, kwa mfano misukule wote aliowatoa Mkoani Tanga wanadaiwa ni wa kutengenezwa ndiyo maana amekuwa mkali kwa waandishi ili wasije kuripoti uwongo huo.
Hata hivyo kwa wakazi mji wa Tanga wamesikitishwa na tukio hilo na kupigwa kwa mwandishi huyo maarufu ambae ni ndugu moja na mtangazaji wa TBC1 Domonic Mokiwa.
0 comments: