CHADEMA HAKUKALIKI VIONGOZI WAZIDI KUJIUZULU-SINGITA NAPO KIMENUKA


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(chadema),Mkoani Singida, Wilfred Kitundu, amejiuzulu rasmi nafasi hiyo akipinga maamuzi ya Kamati Kuu kuwavua nyadhifa za uongozi viiongozi watatu akiwemo Zitto Kabwe aliyekuwa Naibu Katibu Kuu wa Chama hicho. 

Viongozi wengine ni Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba ambao wanadaiwa kukisaliti chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kitundu alisema kinachoendelea ndani ya chama hicho kwa sasa ni udhalilishaji wa demokrasia ya kweli na kuwa ubabaishaji.

Aliongeza kuwa uamuzi aliochukua ni hiari yake bila kushawishiwa na mtu huku akidai kuwa na dhamira ya kulinda  demokrasia ya kweli ili kuhakikisha inatekelezwa kwa vitendo na si kuimbwa tu kwa maneno.
"Mimi ni mwananchama wa kwanza kujiunga na Chadema Mkoani hapa, ninayoheshima kubwa na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa sehemu ya udhalilishaji huu wa demokrasia,"alisema

"Nitaendelea kuwa mwaminifu na mwadilifu ili kuleta haki na Demokrasia siku zote na sitorudi nyuma" alisema M/kiti huyo aliyejiuzulu. Aliongeza kuwa, "Kitendo cha Kumvua nyadhifa za uongozi Zitto Kabwe na wenzake si kizuri na kimeacha maswali mengi yanayoulizwa na wanachama wake,"alisema Kitundu.

Msimamo wa Chadema Mkoani humo(Singida)
Kitundu alisema msimamo wa chama hicho Mkoani humo ni kulaani, kupinga na kukemea maamuzi hayo ambayo yamejaa chuki, hofu na wasiwasi mwingi hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu ndani ya chama.

Katika barua yake ya kujiuzulu ambayo alimwandikia Katibu wa chama hicho Mkoani humo, Kitundu alisema Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe anapaswa kutoa neon ili wanachama na wananchi waendelee kukielewa chama hicho vizuri badala ya kukigawa vipande.

"Msimamo mwingine ni kumtaka Bw Mbowe na Katibu Mkuu Dk Wilbrod Slaa, kuitisha mara moja mkutano wa Baraza Kuu la chama ili kutoa maamuzi ya suala hili kwani lilifanywa na watu wachache kwa maslahi yao,"alisema

Alishauri suala hilo kuwa ni la msingi sana na maamuzi ambayo yanatolewa yanatakiwa kuwa makini ili kudumisha hali ya utulivu ndani ya chama, alioongeza kuwa sababu nyingine kufanaya chama kiendeleze umaarufu wake.
Kitundu mbali na kushika nafasi ya Mwenyekiti wa chama Mkoa, pia aliwahi kuwa muasisi na mlezi wa chadema.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: