SHILOLE ATACHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU BAADA YA KUANIKA CHUPI NA SHANGA ZA KIUNONI HADHARANI..
WENYEKITI
wa Kamati ya Umoja wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, Kimela Billa,
ameutaka uongozi wa Shirikisho la Muziki Tanzania, kumchukulia hatua ya
kinidhamu, msanii wa muziki wa mduara Shilole ambaye pia ni muigizaji wa filamu kwa kosa
la kukiuka maadili ya Tanzania katika tamasha la Serengeti Fiesta,
mkoani Iringa.
Shilole
alipanda jukwaani akiwa anacheza wimbo wake wa ‘Nakomaa na jiji’ huku
akiwa amevaa nguo ambazo zilionesha maumbile yake yote ya mwili.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Billa alisema Shirikisho la muziki chini ya rais
wake, Addo Novemba wanatakiwa kuchukua hatua zaidi juu ya shilole kwa
kosa la kuwadhalilisha wanawake ikiwa ni pamoja na kukiuka maadili ya
Tanzania.
“Hatukatai
hayo mambo yapo lakini kwa staili ile sisi kama viongozi wa sanaa
hatutaweza kuvumilia, shirikisho la muziki wakishindwa kutekeleza hili
lazima kamati ilivalie njuga swala hilo, kiukweli wanalidhalilisha taifa
hawa wasanii, mbona wanaume hafanyi shoo zao uchi,? Alihoji Billa.
Alisema
shirikisho la muziki liige mfano wa shirikisho la filamu kama
lilivowaonya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel kwa makosa kama hayo, ambapo
anamini kwaasilimia kubwa kunachangia kuwa na nidhamu wanapopanda
jukwaani.
“Angekua
ameenda kwa shughuli za filamu wangelifanya wao lakini hili shirikisho
la muziki wanatakiwa wakae meza moja na Shilole kulizungumzia hilo, wao
wanakua wazito kuwachukulia hatua wasanii wa muziki kuliko filamu lakini
kwa hili haitawezekana, ,” alisema.
0 comments: