SHEHENA YA SAMAKI WALIOHARIBIKA YANASWA JIJINI DAR ES SALAAM..
Shehena
ya samaki tani 22.5 kutoka nchini China wanaodaiwa kuharibika na
kutokuwa salama kwa matumizi ya binadamu wamekutwa katika eneo la
Tabata Bima jijini dar es salaam huku baadhi ya samaki hao wakiwa tayari
wamekwishaingizwa sokoni kwa kuuzwa.
Baada ya kuwepo kwa fununu za uingizwaji wa samaki waodaiwa kuharibika kutoka nje ya nchi na kuingia hapa nchini na kuatarisha maisha ya walaji,ITV iliendelea kufuatilia tetesi hizo kwa kushirikiana na maafisa wa mamlaka ya chakula na dawa nchini-Tfda...
Lengo la ufuatiliaji huo lilikuwa ni kuwabaini wahusika wa samaki hao ambapo kwa eneo la tabata bima jijini dar es salaam kontena mbili zilikutwa zikitumika kuhifadhia samaki wa aina tofauti ..

Katika
kontena ya kwanza inayomilikwa na kampuni ya SAIS Boutique inadaiwa
iliingiza samaki aina ya vibua tani 22.5 kutoa china julai 2013 na kwa
bahati mbaya samaki hao wamedaiwa kuharibika licha ya kuwa walishaanza
kuuzwa sokoni tangu walipofika.
Afisa uhusiano wa mamlaka ya chakula na dawa nchini -Tfda Bi Gaudencia Simwanza,ameeleza kusikitishwa kwa uwepo wa samaki hao waliharibika katika kontena hiyo huku akiongeza kuwa kontena nyingine mali ya kampuni ya Amasa Fish Traders iliyokuwa na samaki tani 27 aina ya vibua na kolekole kutoka nchini Yemen lazima ichunguzwe pia ili kubaini usalama wa samaki hao.
Mmiliki wa kontena iliyokutwa na samaki zilizoharibika Bwana Sadick Maporo,alikiri samaki wake kuharibika lakini akadai kuwa samaki hao waliharibika baada ya kufika hapa nchini kutokana na kukatikakatika kwa umeme.
Mamlaka ya chakula na dawa tfda wamedai hawajatoa idhini ya samaki hao kuhifadhiwa katika kontena hizo huku barua iliyoonyeshwa na mmiliki wa kontena hiyo haikuonyesha taarifa ya Tfda kama walikagua samaki hao walipofikishwa hapa nchini jambo linalotia shaka
0 comments: