NAPE AMTAKA MBOWE AJIUZULU HARAKA SANA., AWASHAURI WANANCHI KUTUMIA BUSARA KATIKA UCHAGUZI UJAO.
Katibu wa Itikadi na Uendezi wa Chama Cha mapinduzi (CCM),Nape Nnauye amemtaka Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe kujiuzulu nafasi hiyo mara moja kwa sababu ameshindwa kuiongoza kambi hiyo.
Wito huo uliutoa mjini Shinyanga Ijumaa jioni alipokuwa
akihutubia mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya siku Nne ya
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana katika mkoa huo.
Nape alisema vurugu zilizotokea hivi karibuni
Bungeni ni uthibitisho wa wazi kuwa,Mbowe ameshindwa kuiongoza kambi
hiyo kwa kuwa kabla yake hakukuwahi kuonekana fujo na vurugu kama hizo
katika chombo hicho kinachoheshimika.
Alisema udhaifu wa Mbowe katika kuiongoza kambi
hiyo ndiyo unaosababisha ishindwe kufanya kile ambacho Watanzania
wanakitarajia kutoka kwa wapinzani.
Alisema wanasiasa ambao wanasababisha na kushabikia fujo na vurugu hawafai kwa madai kuwa wanaipeleka nchi mahali pabaya.
Hata hivyo, alisema hilo halitafanikiwa kwa sababu
Serikali, CCM na Watanzania wapo makini dhidi ya mtu yeyote anayepanga
kuwachonganisha. Aliishangaa Chadema kwa kushinikiza wabunge waongezwe
kwenye Bunge la Katiba huku ikitaka wengi wa hao watokane na wanasiasa.
“Chadema inataka wawakilishi wa wakulima wawe kumi
tu wakati wakulima ni asilimia 80 ya Watanzania wote. Hivi kweli wana
lengo la kuwatetea Watanzania au maslahi binafsi tu,?”alihoji Nape.
Nape waliwataka wananchi kufanya uamuzi wa busara wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu .
Nape waliwataka wananchi kufanya uamuzi wa busara wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu .
0 comments: