MWANAMUZIKI WA TAARABU AHMED MGENI AFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI..

Mwimbaji wa kundi la Zanzibar Njema Mordern Taarab Ahmed Mgeni amefariki dunia leo alfajiri (September 17) katika Hospitali ya Mnazi mmoja, Kisiwani Zanzibar alikolazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua.

Akiongea katika kipindi cha Leo Tena ya Clouds Fm mkurugenzi mwenza wa Zanzibar Njema Modern Taarab Ally Ngereja amesema msiba uko Amani Fresh, Zanzibar ambapo ni kwa baba yake na atazikwa leo (September 17) saa kumi jioni.

Marehemu aliwahi kutamba na nyimbo nyingi ikiwemo sitetereki inayofanya vizuri mpaka sasa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: