TCRA YAJIPANGA KUZIFUNGA SIMU ZOTE ZA KICHINA ( SIMU FEKI ).
Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga
simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia
uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.
Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa
sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu
mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.
Zoezi
litaanza kwa kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya zoezi la kuzima
simu kuanza ili kuhakikisha kuwa wananchi hawaathiriwi na zoezi
hilo.
Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na
uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya
mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EP
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: