UPDATE:MADAWA YA KULEVYA CHINA,ASKARI WAVAMIA VYUMBA VYA WABONGO WAPEKUA MADAWA...
CHINA kumekucha! Sakata la kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’
linazidi kulitafuna taifa, safari hii limechukua sura mpya baada ya
askari nchini China kufanya oparesheni maalum ya kuwanasa wahalifu wa
biashara hiyo haramu nchini humo.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichozungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu kutoka China, baada ya vyombo vya habari kuripoti mfululizo juu ya mfumuko wa biashara hiyo, askari waliandaa mpango maalum wa kuwanasa watu wanaojishughulisha nayo.
“Baada ya vyombo vya habari kuripoti
sana juu ya kukithiri kwa biashara ya madawa kulevya, polisi wamecharuka
na kufanya msako wa nguvu katika maeneo ambayo Watanzania na watu
mbalimbali wa kutoka Afrika wanafikia hapa China,” kilisema chanzo
hicho kwa sharti la kutotajwa jina.
Chanzo kilibainisha kuwa, Jumatatu iliyopita wiki hii walifanya msako huo katika mjengo maarufu kwa jina la Dragon polisi walivamia na kuwakuta Wabongo na raia wengine wa kigeni Wanigeria na Waghana.
0 comments: