Wema Sepetu "Mimi na Wanaume tu, Siwezi Badilisha Hii Style"
Wema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Endless Fame, anadaiwa kuwa beneti na kijana aitwaye Robby lakini mwenyewe amesema kwamba hakuna anayeweza kumtenganisha na wanaume.Habari zinasema kuwa, Wema na Robby wamekuwa wakipiga picha za kimahaba na mnyange huyo kuziingiza kwenye mtandoa wake na kumtambulisha kijana huyo kwa jina la ‘Honey’
Risasi Jumamosi lilifanya juu chini na kumsaka Wema ili kumtaka ajibu tuhuma za kuwa katika mahaba na kijana huyo.
Mei 22 mwaka huu, mwandishi wa gazeti hili alifika ofisini kwa mrembo huyo, Mwananyamala Komakoma jijini Dar es salaam na kumbana kwa maswali juu ya kuvuja kwa picha zake hizo akiwa na Robby na nyingine akiwa na wanaume wengine tofauti.
“Watu wamekuwa wakinizungumzia kila kukicha, tena maongezi yao yamekuwa yakianzia kwenye baadhi ya picha zangu, kila mtu ana namna ya kutengeneza ‘laifu’ yake na miye huwa sioni shida mwanaume asiye hawara yangu kunikisi au miye kumkisi,” alianza kujitetea.
“Ukifuatilia historia yangu mara nyingi utagundua marafiki zangu wengi ni wanaume kuliko wanawake na wengi wao wanakuja kwangu, tunakunywa na wanaondoka mida mibovu, kwa asiyenijua anaweza kuhisi ni mabwana zangu kumbe siyo, hata kwenye mitandao huwa sioni tabu kuweka picha za mtu akinikisi au nikimkisi,” aliendelea kusema.
“Siwezi kubadilika hii ni life style yangu. Siwezi kuacha kuwa karibu na marafiki wa kiume, hivyo ndivyo nilivyoumbwa watu wasinishangae, suala la kukutana na mtu na kupiga naye picha siyo ishu kwangu, ningekuwa mtu wa ajabu sana kama ningekuwa nawakisi midomoni au wao kunikisi mdomoni,” aliongeza.
Wema amesema kuwa watu wana hisia mbaya juu yake na Robby jambo ambalo siyo sahihi kwa kuwa, katika maisha yake anawapenda marafiki wa kiume zaidi ya wanawake.
NDIYO HUWEZI CI UNAPEPO LA NGONO?WEMA SEPETOOO HAUFAIII DADAETU WANAOKUSHOBOKEA HAWANA AKILI,KAMA NI CHUMA WE SIKIREPA SHANGAZII
ReplyDelete