KIJANA ANUSURIKA KUFA BAADA YA VIBAKA KUMCHOMA MOTO HUKO LINDI
Friday, May 31, 2013 | 6:52 PM
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ismai Mayoba(31) anayefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Manispaa ya Lindi amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto.
Kwa sasa kijana huyo amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo.
Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.
Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndugu Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie Moto huku akijua ni kosa kisheria.
Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo
0 comments: