KUFURU:MAPOLISI DUBAI HUTUMIA LAMBORGINI NA FERRARI KUFANYA DORIA



Amini usiamini brand za magari zilizojaa katika garage ya polisi ya Dubai ni Lamborgini, McLaren MP4-12C, Aston Martin, Ferrari, Bentley na Chevrolet.
Mwaka jana tuliwahi kuandika kuhusu chuo cha Dubai ‘American University in Dubai’ chenyewanafunzi wengi wanaomiliki magari ya kifahari duniani, lakini sasa ni polisi wa Dubai ambao wamenunuliwa magari hayo kwaajili ya kufanya patrol za kawaida mitaani.
Dubai-police-cars4
Hata maaskari wenyewe wa Dubai wamekiri kuchanganyikiwa baada ya kupewa magari hayo kwaajili ya kufanyia kazi.
Dubai-police-cars5
Mmoja wa askari hao aitwaye Mariam Ahmed, ambaye binafsi anamiliki Toyota Land Cruiser amesema alipokabidhiwa kuendesha Ferrari FF kwaajili ya doria mitaani hakuamini, na huwa anatamani asipate Off awe kazini muda wote sababu ana enjoy kuwa kwenye Lamborgini awapo zamu.
“Ni mara yangu ya kwanza kuendesha Sport car”, alisema “waliponichagua sikuamini, ni raha sana kuiendesha, nikiwa off huwa naimiss sana siwezi kuifananisha na Land Cruiser yangu”.
Dubai-police-cars7
Aliongeza, “inafurahisha sababu kuna watu huwa wanatuomba tuwakamate kwa sababu yoyote ya kubambikiza ili tu wapande Ferrari wakati wa kwenda polisi”.
Dubai-police-cars8
Askari mwingine aitwaye Abdullah Mohammed , alisema magari hayo yamewaongezea ujiko wanapokuwa wanayaendesha mitaani.
“Kinachofurahisha zaidi katika kuendesha gari kama hiyo ya kifahari ni jinsi watu wanavyokutazama na tabasamu kubwa”.
Dubai-police-cars9
Kwa mujibu wa GeeksTopten Dubai ndio inakamata nafasi ya kwanza katika Top 10 ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na magari ya polisi ya gharama zaidi 2014, ‘Top 10 Countries Having Most Expensive Police Cars in 2014’.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: