IZZO BUSINESS ALIGOMA KUMPIGIA KAMPENI RIDHIWANI JAPO ALIOMBWA KUFANYA HIVYO


Jumapili iliyopita (April 6), Ridhiwani Kikwete alitangazwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi wa kiti cha ubungo wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani.

Hii ilikuwa habari njema pia kwa Izzo Bizness ambaye aliwahi kumuimbia mbunge huyo ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete akimtaka aongee na ‘mshua’ kuhusu hali halisi ya mtaani.

Izzo Bizness ameuambia mtandao wa Bongo5 kuwa tangu atoe wimbo huo amekuwa karibu na Ridhiwani kimawasiliano na hata wakati wa kampenzi za ubunge wa jimbo la Chalinze alimuomba amsaidie lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na hali ilivyokuwa kwa upande wake.

“Kuna vitu vidogo tu ambavyo tulipishana, niliangalia pia katika upande wangu. Hakikuwa kitu cha kusaidiana kimasihala kwa kuwa unapoamua kuingia kwenye kampeni kumsaidia mtu ujue ushaamua kutake risk. Na hapo mimi nilikuwa naenda kukipa tafu chama cha CCM lakini mimi natokea jimbo ambalo limeshikiliwa na CHADEMA na wananchi asilimia kubwa ni CHADEMA”. Amesema Izzo Bizness.

Source: Bongo5
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: