CHADEMA INAPOTEZA MWELEKEO NA KUFA KIFO CHA MENDE KWA KUKOSA WASHAURI


Hakika kila mtu na kila kiongozi hasa mwenye mamlaka makubwa ni busara kuwa na WASHAURI ambao watamshauri na kumkosoa pia kabla ama baada ya kufanya maamuzi katika uongozi wake. Hili lipo wazi hata familia yenye baba, mama na watoto, baba anaweza kutafuta mshauri pembeni kuhusu namna ya kuiongoza familia.

Ni muda mrefu huwa najiuliza hili swali, hivi washauri wa Dr. Slaa na Mbowe ni kina nani maana nahc kama hawana ndio maana wanafanya maamuzi yasiyo sahihi kila wakati kwakuwa maamuzi hayo hayajengi wala kuleta maendeleo ndani ya Chadema. Mfano; timua timua za viongozi katika chama, kufanya utalii kwa chopa, kukataa kukaguliwa hesabu, kupanga maandamano yasiyo na tija, kususia vikao halali vya bunge, n.k. 

Haya yote yasingepelekea chadema kufa kifo cha mende kama wangekuwa na washuri wa chama. Wanawapuuza wazee kama Ndessa na Mtei, wanatumia halmashauri za vichwa vyao wenyewe, matokeo yake ndio hayo. Na kama wanao washauri, itakuwa hao wanaowashauri wanawashauri vibaya.

Kwani Mbowe akiwaza jambo lake, anawaita akina Lema, Lissu na wanachama wengine na waandishi wa habari wanaweka mikakati ya kulitekeleza pasipo kupingwa! Lifanikiwe, lisifanikiwe, akiota lingine anafanya vivyo hivyo.
Dr. Slaa nae hivyo hivyo, akiwaza kitu chake, fasta anaita waandishi wa habari na baadhi ya viongozi na wanachama isipokuwa Lema, maana lema wanadharauliana, wanaweka mikakati ya kutekeleza jambo hilo mara moja bila kupingwa!
Hawana team work ndo maana wanaishia kutimuana!

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: