TATHMINI YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MADIWANI BAADA YA CCM KUIBUKA KIDEDEA JANA



Hakika nimepata mshituko mkubwa kuona matokeo ya uchaguzi wa udiwani katika kata mbalimbali yameenda ndivyo sivyo kwa upande wa chadema. Katika kata 27 ukitoa 1 zinabaki 26.

Katika kata hizi CHADEMA imepata kata 3 tu huku NCCR ikiendelea kupata hisani ya kata 1 kwenye Jimbo la Zitto Kabwe. Zilizobakia zote CCM imechukua. Sasa hapa ndipo mshituko wangu ulipoanzia.

Lakini zipo sababu kadhaa zilizopelekea matokeo haya.CHADEMA na ujazaji wa watu kwenye mikutano yake Itakumbukwa kwamba hivi karibuni uongozi wote wa juu ulipita katika mikoa kadhaa kufanya mikutano na wananchi.

Japo agenda kuu haikuwa uchaguzi huu wa madiwani lakini walitumia nafasi hiyo pia kuwanadai wagombea udiwani wake. Kwa mahudhurio tuliyokuwa tunayaona kupitia ITV na mitandao ya kijamii tungeamini kuwa hii ilikuwa nafasi ya ushindi wa kishindo safari hii. Lakini mambo yameshtua zaidi. Nadhani tujitatmini upya.

Tubadilishe mbinu za kushambulia adui. Je wahudhuriaji wote ni wapiga kura? Nilichobaini kwa mtazamo wangu ni kuwa wale wote wanohudhuria mikutano ya CHADEMA si wapiga kura halali wanaotambulika na NEC. Wale ni wapiga kura wetu wasio rasmi. 

Chukua mfano wa kata ya Nyasura huko Bunda ambayo tuliambiwa toka awali kuwa tayari CCM ipo katika hali mbaya. Lakini matokeo yamekuwa tofauti. Labda palipokuwa na ukweli ni huko Njombe mjini tu ambako CHADEMA imeshinda. Nini tatizo hapa? Kwa mtazamo wa haraka haraka unakubaliana na hoja ya CHADEMA waliyokuwa wanaililia.

Hoja ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura. Hapa ndipo CCM ilipokuwa inatumia mwanya adhimu kabisa. Ni ukweli kuwa kuna wananchi wengi hawana vitambulisho vya kupigia kura. Vijana wengi nawafahamu katika eneo langu ambao ni wakereketwa wa CHADEMA hawana vitambulisho hivi.

Kwa hiyo basi, Tume ya Uchaguzi itakapoliboresha daftari hili naamini Chadema itapata mtaji mkubwa mkononi. CCM ina wapiga kura? Ndio.Hapana. Majibu yote ni sahihi kwa sasa. 

CCM ina wanachama na wapiga kura waliozeeka. Kwanini? Ukiwatazama wapiga kura wengi wa CCM ni wale wanachama wao ambao si wengi. Lakini wanafanikiwa kupata kura hizo kwa sababu CHADEMA haina wapiga kura wa kutosha ukilinganisha na idadi kamili ya wahudhuriaji wa mikutano yake.

Akina mama ndio wapiga kura namba moja kwa CCM. Idadi hii itazidiwa pindi daftari la wapiga kura litakpoboeshwa. Ni kweli CCM inanunua wapiga kura? yawezekana kweli lakini binafsi napingana na hoja hii. 

Hivi tunaposema wananunua wapiga kura kwa kuchukua shahada zao, wao wenyewe wahusika wanakuwa wamejitoa ufahamu? Madai haya nayasikia kwa muda mrefu sana. Lakini mbona mimi katika eneo langu hawaji kunishawishi kununua hiyo shahada? Au wanaangalia na mtu mwenyewe wakiona unajitambua wanakuruka? Wananchi ndio wajinga kwa kukubali kuuza shahada hizo kwa bei ya kujidhalilisha. 

Ushauri wangu CHADEMA tujipange upya. Tujitathmini. Kwa mwenendo ninaouona kwa sasa, chaguzi za serikali za mitaa tutapata aibu kubwa na hapo ndipo ndoto ya Ikulu itakapoyeyuka.

Nimeshauri sana kwa baadhi ya viongozi wa mkoa kujikita zaidi vijijini ambako mwamko umeanza kujitokeza kwa kuunga mkono upinzani. Sasa tusiwakatishe tamaa. Viongozi hatupendi kwenda kufanya mikutano vijijini.

Tayari mjini watu wameshaelewa umuhimu. Tusahihishe makosa yetu. Kipimo kikuuu cha CHADEMA kuingia Ikulu kitatokana na namna tutakavyojipanga kwenye serikali za mitaa. Hadi hivi sasa tunakosa wagombea wa serikali za mitaa. Hatujajipanga. Tukiendelea kulalamika tu kwa mbinu chafu wanazofanya CCM tutaishia kulia kila siku.

Kumbukeni kuwa Jeshi la Polisi hasa viongozi wake wakuu wote wapo CCM. Huwezi kupata cheo serikalini kwa sasa kama wewe si mwanachama wa CCM.

Hivyo basi, kufikiri jeshi la polisi hasa viongozi wake kuunga mkono upinzani ni ndoto kubwa ambayo hatupaswi kuota usiku wala mchana. Ni hayo tu kwa sasa. Nimesikitika sana kwa matokeo haya.
Source:Ngalikivembu wa JF
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: