NAPE"CHADEMA NI MZIGO KWA TAIFA"
Chama ca Mapinduzi (CCM) kimewashukuru watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika kata 27 na kushinda kata 23.
Kimesema siri ya kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi tosha kwamba hakikubaliki na Watanzania.
Katibu wa NEC ya CCM, Itkadi na Uenezi, Nape Nauye, amesema hayo na kuongeza kuwa matokeo hayo ni ushindi kwamba CCM inakubalika zaidi na Watanzania wengi.
Akizunguma kushindwa kwa CHADEMA, amesema wamehukumiwa kutokana na vurugu za kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi ndiyo maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.
“Watanzania hawapendi vurugu wamezoea Amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini chama hicho,” amesema.
Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata 23 za Kibinduna Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura (Mara), Malindo na santillya (Mbeya). Zingine ni Partimbo (Manyara), Mkwiti ( Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro) na Mrijo ( Dodoma).
Source, Uhuru

0 comments: