Mwanafunzi abakwa kikatili mkoani Singida....Sehemu zake za siri na makalio vyote vimeoza na vinatoa usaha...soma zaidi hapa


 



 
Mwanafunzi  wa kike,13, (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la tano katika shule ya Msingi Unyakumi, mkoani Singida, amefanyiwa unyama kwa kubakwa na kijana aliyemtaja kwa jina moja la Mapunda ambaye ni dereva wa bodaboda.

Akizungumza kwa shida kutokana na maumivu makali aliyonayo akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, denti huyo alisema kwamba mkasa huo ulimpata Novemba 19, mwaka huu wakati akitoka shule akielekea nyumbami kwao.
 
Akisimulia mkasa huo mwanafunzi huyo alikuwa na haya ya kusema:
 
“Mimi ni mtoto yatima wa kufiwa na baba, mama naye aliachana na baba nikiwa na umri mdogo, nimekulia katika shida tena kwa kulelewa na watu tofautitofauti, niliona kitakachonikomboa ni elimu lakini ndoto yangu sasa imekufa.
 
“Imekufa kwa kuwa nateseka kitandani kwa muda mrefu sasa kutokana na maumivu yaliyotokana na kubakwa.Nimekua wa kujisaidia kitandani, nawakumbuka wazazi wangu, leo hii wangekuwepo wangekua watetezi wagu, sina uhakika kama nitapona na kwenda shule tena.
 
“Kutoka shuleni hadi nyumbani ni mwendo wa saa moja, siku hiyo niliyobakwa ilikua Ijumaa, nilikua natoka shule nikielekea nyumbani, njiani kuna vichaka na mashamba ya mikorosho, nilipofika karibu na banda bovu nilimkuta kijana amekaa juu ya jiwe.

“Nilijisikia vizuri sana nilipomuona, uoga ulinitoka juu ya wanyama wakali, sikua na hofu ya aina yoyote kama angenigeuka, nilipomkaribia alinikamata kwa nguvu, alinivuta akanipeleka katika banda bovu.
“Nilijaribu kujinasua lakini nilishindwa kwani alikua na nguvu kuliko mimi, niliamua kupiga kelele ili nipate msaada toka kwa mtu yeyote anayepita, hata hivyo, hakuna aliyejitokeza, alinifunika mdomo, alinipiga, niliishiwa nguvu, akaniingilia, alipomaliza haja yake, akakimbilia pasipojulikana.
 
“Nilitokwa damu nyingi zilizotoka sehemu za siri, niliinuka na kutembea kwa shida kwani hata kiuno kilikua kikiuma sana, nilifika nyumbani, sikumkuta dada kwani alikuwa ana kawaida ya kurudi usiku akitokea kazini kwake.
 
“Aliporudi alikuta nimeshafua nguo zangu na nimeshalala, niliona aibu kumweleza, ilipofika Jumapili maumivu ya kiuno na sehemu za siri yakaongezeka, nilikua nikitembea kwa shida, ilimbidi dada aniulize nina nini? Awali niliogopa kumweleza lakini baadaye nilimsimulia kila kitu kwani maumivu yalizidi.
 
“Nilishindwa hata kwenda shule, nilipelekwa hosptali ya wilaya lakini hali yangu ilizidi kuwa mbaya. Nikahamishiwa hospitali ya mkoa, Singida lakini sikuweza kupata nafuu, nikaletwa hapa Muhimbili kwa gari la wagonjwa ‘ambulance’ kwani nilishindwa kukaa kwenye  kiti cha basi.
 
“Bado sijaweza kukaa wala kuinuka, hata kulala kwangu ni kifudifudi, nalishwa, naogeshwa kitandani, kwa kweli sina raha hata kidogo tangu nifanyiwe unyama huo maana sijaenda shule, wenzangu wamefanya mitihani mie sipo, nauguza mamivu.
 
“Nimeoza sehemu za siri hadi makalio, natokwa na usaha, siamini kama nitapona na kwenda shule tena. Aliyenitenda haya tunaishi naye mtaa mmoja na hajawahi kunitongoza ila aliamua kunibaka.
 
“Nimefikishwa hapa Muhimbili Novemba 20, mwaka huu, naomba taarifa hizi zimfikie mama popote alipo kwani aliachana na baba akarudi kwao Musoma,”alieleza kwa uchungu denti huyo.
 
Dada wa mtoto huyo anayeishi naye aliyejitambua kwa jina moja la Rose alipoulizwa juu ya madai hayo alikiri kutokea na ameiomba serikali imkamate mtuhumiwa ili haki itendeke.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: