AFISA UTUMISHI WA MANISPAA YA ILEMELA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA YA NGONO ...

 

 Afisa  utumishi  wa  manispaa  ya  Ilemela  ndugu Songoma  leo  amefikishwa  mahakamani  akikabiliwa  na  kesi  ya  rushwa  ya  ngono  kwa  mwalimu  aliyekuwa  akiomba  kuhamishwa  toka  Ngudu  kuja  Mwanza.

Akisomewa  shitaka  lake   mbele  ya   hakimu  mfawidhi  wa  mahakama  ya  Mwanza, ofisa  wa  TAKUKURU  Bi. Debora amedai  kuwa   Songoma  alitenda   kosa  hilo  may  tano  mwaka  jana  ambapo  maofisa  wa  TAKUKURU  walifanikiwa  kumtia  mbaroni  wakati  akijiandaa kupokea  rushwa  ya  ngono ndani  ya  gesti  moja  jijini  mwanza  katika  mtego  ambao  uliandaliwa  na  mwalimu  huyo.

Hata  hivyo, Afisa  huyo  amekana  shitaka  hilo  na  kesi  yake  imeahirishwa  hadi  septemba  13  mwaka  huu.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: