MUME ATOROKA BAADA YA MKE KUZAA MAPACHA WATATU,NI KUTOKANA NA UGUMU WA MAISHA HUKO NIGERIA...!!

 

Mkulima mwenye umri wa miaka 40, Biodun Akapo, mkazi wa Kijiji cha Afojupa, kitongoji cha mji wa Owode-Egba la Jimbo la Ogun, akimbia kwa sababu mke wake amezaa mapacha watatu.

Mama huyo alijifungua mnamo Julai 24 na alikuwa na uwezo wa kulipa bili tu ya hospitali tena  kwa kuingilia kati na mtawala wa jadi wa mji, Kolawole Sowemimo.

Akisimulia mkasa huo,Bose Akapo mwenye umri wa miaka 30, ambaye tayari ana watoto wawili wenye umri wa miaka 5 na 8, alisema mume wake hakuwepo nyumbani alipoanza kujisikia uchungu. Alieleza kwamba yeye alisaidiwa na jirani yake aliye mpeleka hospitali na pikipiki.

Alisema  kuwa yeye hakujua kuwa alikuwa na watoto watatu tumboni mwake.

'Mimi nilipelekwa hospitali na pikipiki ya jirani,nilipoanza kuona ishara ya kujifungua, kwa sababu mume wangu hakuwepo nyumbani . Lakini cha kushangaza, Nilizaa mapacha watatu na habari zilipomfikia mume wangu hakuja kuniona mpaka sasa hivi,

Mama huyo  alisema ilimbidi awasiliane na mtawala wa jadi wa Owode-Egba, ambaye alimpa  msaada wa mavazi na vifaa vingine vya matibabu kwa watoto

Amlaumu mume wake kwa kumtelekeza baada ya kusikia kuwa amezaa mapacha watatu,atoroka na hajarudi

Mama wa nyumbani, indigene Ibadan kama mumewe, alisema wamekuwa wakiishi pamoja  kwa furaha kijijini kwao kwa zaidi ya miaka kumi. Yeye aliomba na mumewe arudi nyumbani.

'Mimi hata sijui yuko wapi mpaka sasa, lakini namuomba arudi nyumbani kwa ajili ya watoto hawa wasio na hatia' Bi Akapo alisema.

Pia alitumia nafasi hiyo kukata rufaa serikalini, watu binafsi, vikundi mbalimbali kuomba misaada  kwa ajili ya kulea  watoto hao, na ajira ili apunguze ugumu wa maisha.

Mama na mapacha wake watatu wako katika hali nzuri kiafya na wameruhusiwa kutoka hospitalini.

Akizungumza juu ya maendeleo, mtawala wa jadi alimshukuru Mungu kwa ajili ya kujifungua salama, na pia alitoa wito kwa serikali na Wanigeria wengine kutoa misaada ili kuwalea watoto hao.

Mheshimiwa Sowemimo alionyesha matumaini kwamba serikali itahudumia  mahitaji ya familia ya utawala huo unaojulikana kwa maisha ya wananchi na wakazi.


TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: