VIFO VYA WASANII... DOKII: MUNGU ANATUADHIBU KWA MABAYA YETU...!!

MWIGIZAJI Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ameibuka na kusema kuwa vifo vya wasanii vimetokea kutokana na kujisahau hivyo Mungu ameamua kuwaadhibu. Akichonga na paparazi wetu katika Viwanja vya Leaders Club, Juni 5, mwaka huu ambapo mwili wa Mangwea ulikuwa ukiagwa, Dokii alisema matukio ya vifo vya wasanii mbalimbali yaliyotokea miaka miwili mfululizo ni pigo kubwa kwani wengi ni vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kitu ambacho anakiona ni ishara kuwa Mungu anataka kujidhihirisha kwa wasanii.

“Wasanii tulijisahau sana na kuona Mungu hayupo kwani kipindi bado hatujatoka na tunatafuta kutoka kisanaa, tulikuwa tunamuomba kila wakati lakini baada ya kutoka na kuwa mastaa tumemsahau kabisa.
“Hatukumbuki kwenda ibadani tunabaki kuendekeza starehe za dunia tu, hivyo tubadilike kwani Mungu ameanza kujionesha kwetu kwamba yupo,” alisema Dokii.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

1 comment:

  1. Dokii umenena, ila siku hizi uko wapi hatukuoni katika nynaja za kawaida, za kuigiza, kuimba na nyingine. Jitokeze ulielimisha sana enzi hizo, au nielekeze unapatikana katika nyanja zipi?

    Itakuwa vema tuwasiliane mtani

    ReplyDelete