Vitu Vinavyofanya Kuyachukia Mapenzi na Kutotamani Kuolewa ama Kuoa

Kutokana na maumivu yanayo sababishwa na mapenzi kuna wengine kati yetu wameshakata taama ya kuingia tena kwenye uringo wa mahusiano, ninapozungumzia maumivu kwa wale ambao yamesha watokea wananielewa vizuri sana, zile hali za kutokula na nakukonda zikisindikizwa na machozi ni kawaida.

Hali hiyo imesababisha kujenga hofu mioyoni, japo wengine hofu zao hazitokani na maumivu ya mapenzi, katika hilo kila mmoja ana vile anavyo ijenga hofu, labda kutokana na mziki anao sikiliza, ,stori, mitandao, majarida na movies mbali mbali zinazo zungumzia maumivu ya kimapenzi na jinsi watu wanavyo teseka.

Mfano kama mimi wakati naanza mapenzi nilikutana na binti ambae tayari alikuwa ni mwenyeji katika eneo hili la mapenzi, kwa ugeni wangu nilijiweka kumbe wenzangu kuchepuka kwake yeye nikawaida tu iliniumiza sana na mapenzi yakaishia hapo, nikajenga hofu kwamba hakuna msichana mwaminifu, baada ya kuanzisha mahusiano na binti mwingine sikuona sababu ya kuwa na mmoja nikawa na kula vichwa kama kinyozi siku zinasonga ikafikia hatua mama yangu akawa ananiita kiwembe, nilipoingia katika harakati za kujitegemea kimaisha nikajiuliza mawili matatu nikaona huo mpango sio, nikatafuta mmoja akawa permanent nilimuamini sana nikaishi nae kwa muda mrefu, sijui alichanganyikiwa na nini akachepuka bahati mbaya akapewa mimba na huyo jamaa hapo ndo ikawa mwisho wa ukrasa.(ni ushuhuda sijisifii)

Sikukata tamaa nikatafuta chimbo jipya basi nikawekeza tena moyo, hapa naona mambo sio mabaya mapenzi ya kweli yapo kiasi cha kutia matumaini.

Kiukweli mapenzi ya siku hizi yanatia hofu sana, kila mara mtu unapofikiria kuingia katika mapenzi au kuoa unawaza kwa kuangalia mabinti wa kisasa vijana wa kisasa unahofu hakuna muoaji hapa wala muolewaji, usijenge hofu kutoka na yale ulio pitia na kuyaona, wa ukweli wapo, tabia ya Amina sio ya Veronica na tabia ya Frank sio ya Abdullah.

Leo naomba utoea hofu yako kwa kuandika hapa kwa kifupi kile ambao unahisi kina kukatisha tamaa ya kuoa, kuolewa au kuingia katika mapenzi, na usijaribu kuingia katika ndoa ukiwa bado umezibeba hofu utaukosesha moyo wako amani. Tupeane uzoefu kutoka kwa wale ambao wameshaingia katika mahusiano ya kimapenzi walio oa na kuolewa, pia wamefanikiwa kuyaendesha mahusiano katika misingi ya uaminifu na upendo wa dhati.

Pia kama hofu yako inatokana na mziki, movie na n.k, kama nilivyoelezea hapo mwanzo sema wenda kuna mtu yalisha mkuta atakuquote akupe uzoefu jinsi ya kukabiliana na hali hiyo kwa njia moja au nyingene utakuwa umejifunza
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: