TAZAMA PICHA HIZI ZINAZOONYESHA TASWIRA YA TRENI ILIYOPINDUKA NA KUUA


Wafanyakazi walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa kuamkia katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa. Katika ajali hiyo watu wawili wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa.
Sehemu ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo hayakusombwa na maji katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya Gulwe, hiyo imetokea saa 9.15 usiku. Treni hiyo ya Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam na kuelekea Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa yaliyobeba ngano, sukari na mafuta.

Njia ya Reli iliyoondolewa na maji katika stesheni ya Gulwe Wilaya ya Mpwampwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneno mbambali nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akitoka kwenye maji baada ya kuangalia kichwa cha treni kilichopata ajali na kusombwa na maji katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa, usiku wa kuamkia leo, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali za nchi. Ajali hiyo imesababisha kifo cha watu wawili na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa iliyoko wilayani Mpwampwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk, Shaaban Mwinjaka akimfariji mmoja wa Majeruhi wa Ajali ya treni ya mizigo iliyotokea katika Stesheni ya Gulwe Bw. Michael Lupatu wakati alipomtembelea katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Wilayani Mpwampwa leo mchana. Ajali hiyo ya treni ya mizigo imetokea usiku wa kuamkia leo na kusababisha kifo cha watu wawili na wengine saba kujeruhiwa.
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini uchukuzi)
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: